.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 31 Januari 2015

FRIENDS RANGERS YAPOTEZA MECHI KWA KUGOMA

Mechi namba 120 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kundi A kati ya Majimaji na Friends Rangers iliyochezwa juzi (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilivunjika dakika ya 38 baada ya Friends Rangers kugoma kuendelea na mchezo.

Kwa kitendo hicho, Friends Rangers imepoteza mchezo huo. Hatua nyingine za kikanuni zitafuata baada ya kamati inayohusika kukutana.

Wakati huo huo, mechi ya FDL kundi A iliyochezwa jana (Januari 30 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kati ya African Lyon na Ashanti United imemalizika kwa sare ya bao 1-1.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni