.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 31 Januari 2015

MTAALAM WA SILAHA ZA KEMIKALI WA KUNDI LA IS AUWAWA NCHINI IRAK

Mtaalam wa silaha za kemikali wa kundi hatari la Dola ya Kiislam (IS) nchini Irak ameuwawa katika mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na Marekani na washirika wake.

Marekani imesema mtaalam huyo Abu Malik alikuwa akitoa mafunzo kwa IS, ya kuwawezesha kufanikisha kuwa na uwezo wa kutengeneza silaha za kemikali.

Malik alikuwa ni mhandisi wa silaha za kemikali katika utawala wa rais Saddam Hussein, kabla ya kujiunga na al-Qaeda nchini Irak na baadae kujiunga na IS.

Marekani na washirika wake wamefanya mashambulizi ya anga yapatao 2,000 yanalolilenga kundi la IS.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni