.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 31 Januari 2015

UZINDUZI WA MASJID TAQWA CHUKWANI ZANZIBAR

Masjid Taqwa Chukwani Unguja uliojengwa kwa Nguvu za Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, uliopewa jina na Mufti wa Zanzibar baada ya kuufungua rasmin baada ya ujenzi wake na kujulikana kwa Jina la Masjid Taqwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Chukwani Zanzibar.
                                   Sehemu ya ndani ya Kasjid hiyo kama inmavyoonekana.

Viongozi wa Kamati ya Ujenzi wa Masjid Taqwa wakiwa katika harakati za kupokea wageni.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho akisalimiana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Omar Saleh Kabi alipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuufungua Masjid Taquwa uliojengwa na Wawakilishi na Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi kwa kutowa michango na kufanikisha ujenzi huo na kleo kufunguliwa rasmin kwa ajili ya Ibaada.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakisoma dua baada ya Sala wakati wa uzinduzi wa msikiti huo ulioko katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Afisa Uhusiano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg.Himid Choko, akisoma utaratibu wa hafla ya uzinduzi Masjid Taquwa Chukwani Unguja
Qur-aan ikisomwa na Shekh kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar wakati wa ufunguzi wa masikiti huo ulioko katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Ujenzi wa Masjid Taquwa na Mkuu wa Utawala wa Ofisi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg. Amour Mohammed, akitowa maelezom ya ujenzi huo uliokamilisha kwa michango ya Wawakilishi na Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Shekh, Thabit Nomani Jongoo akitowa mawaidha kabla ufunguzi wa Masj.id Taquwa Chukwani Zanzibar, masjid hiyo imefunguliwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kabi
Mpika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho akizungumza wakati wa ufunguzi wa masjid Taquwa uliojengwa kwa michango ya Wawakilishi na Wafanyakazi wa Baraza Wawakilishi Zanzibar.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Omar Saleh Kabi akiwahutubia waumini wa Dini ya Kiislam wakati wa ufunguzi wa Masjid Taquwa alioupa jina hilo wakati akiufungua rasmin na kuuita jina hilo. Mufti ametowa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam katika uzinduzi huo na kutoa hadithi za Mitume.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwa waumini wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Taquwa Chukwani Zanzibar.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis, akisoma dua baada ya ufunguzi wa Masjid Taquwa Chukwani Zanzibar.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni