.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 30 Januari 2015

WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA MH. WASIRA ASEMA BENKI YA KILIMO KUKOPESHA PEMBEJEO

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Profesa Andrew Temu akisisitiza jambo katika warsha hiyo.
 
Naibu Katibu Mkuu Mkuu Wizara ya Fedha Profesa Adolph Mkenda akichangia mada katika uzinduzi wa warsha iliyoandaliwa na benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Sophia Kaduma akifungua warsha ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADF) iliyofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Sophia Kaduma akiwa na Menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADF), mara baada ya kuzindua warsha kujadili mpango wa maendeleo wa miaka 25 ya benki hiyo.

SERIKALI imesema itaiwezesha benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo ili iweze kutoa mikopo ya pembejeo ili kuweza kunyanyua kilimo na wakulima kwa ujumla.

Ahadi hiyo ya serikali imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Sophia Kaduma ambaye alimwakilisha Waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wasira wakati wa ufunguzi wa warsha ya mpango mkakati wa miaka 25 wa benki hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

“Hakuna nchi duniani ambayo imeweza kubadilisha kilimo bila kuwa na mikopo kwa wakulima, kwa vile teknolojia ya ya kuboresha kilimo ina bei na kwa vile wakulima wengi hawana mitaji.

“ TADB lazima iwe chanzo cha mtaji kwa wakulima na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kuondoa umasikini uliojikita zaidi vijijini hususani kwa wakulima wadogo.”

Alisema serikali ina wajibu wa kuwekeza katika utafiti, huduma za ugani, miundo mbinu ya masoko na uchukuzi na hata umwagiliaji.

Alisema wamekubaliana na menejimenti ya TADB kukutana baada kumalizika kwa vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.

Akizungumza kabla ya Waziri, Mkurugenzi wa benki hiyo, Thomas Samkyi alisema wajibu wao ni kuhakikisha wanaongeza thamani viwanda, kuboresha miundo mbinu katika vijiji kubadili kilimo kutoka katika matumizi ya kawaida kwenda kwenye biashara.

Benki hiyo iko kwenye hatua za mwisho kupata leseni ya kudumu ambapo inatarajiwa kupatikana baadae mwaka huu na kwamba taratibu zote za kuanzishwa kwake zimeshakamilika ikiwepo pia kuajiriwa wafanyakazi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni