Iwapo utapatiwa kikombe cha kahawa iliyochanganywa na kijiko kimoja cha chai chenye siagi na mafuta ya nazi, huenda mtu ukapatwa na mshtuko wa moyo kutokana na mchanganyiko huo.
Lakini baada ya watafiti kubaini
kuwa mafuta ni mazuri kwa binadamu kuliko sukari, na mchanganyiko huo
unasaidia kupunguza mafuta mwilini, sasa kahawa hiyo imejipatia
umaarufu nchini Marekani na Uingereza.
Wapenzi wa mchanganyiko huo wa
kahawa na siagi, wamedai kuwa huwafanya wajihisi wamepata kifungua
kinywa kilichokamilika na hupata nguvu, uongeza umakini, hupunguza
kalori mwilini na kuondoa mafuta ya ziada mwilini na kujisikia shibe
hadi mchana.
Kisu chenye siagi ambayo huchanganywa katika kikombe cha kahawa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni