.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 26 Februari 2015

LIGI YA MABINGWA ULAYA, ARSENAL YATANDIKWA 3-1 NA MONACO

Arsenal imekuwa na usiku mbaya, baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa wageni wao Monaco waliosafiri kutoka nchini Ufaransa, katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
 Wakicheza mbele ya mashabiki wao waliokuwa wamefurika katika uwanja wa Emirates, Arsenal walijikuta wakikubali nyavu zao kutikiswa mara tatu kupitia kwa mabao yaliyofungwa na Geoffrey Kondogbia dakika ya 38, bao la pili la Monaco likifungwa na Dimitar Berbatov dakika ya 53.

Bao la tatau likifungwa na Ferreira Carrasco (90+4). Bao pekee la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Alex Oxlade Chamberlain dakika ya 91.
 Kocha mkuu wa Arseanl, Arsene Wenger ( katikati ) na benchi lake la ufundi wakiwa hawaamini kinachotokea mbele yao.


 Mashabiki wa Monaco waliosafiri kutoka Ufaransa kwenda London kuishangilia timu yao dhidi ya Arsenal

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni