Mwanaume mmoja raia wa Sierra Leone
ambaye alikuwa anafanyakazi katika kituo cha kulelea yatima wa Ebola
amefariki kwa ugonjwa huo wa Ebola.
Mtumishi huyo wa kituo hicho
Augustine Baker alilazwa katika kituo cha kutibu Ebola, baada ya
kuugua wiki iliyopita.
Baker alikuwa akifanya kazi katika
kituo hicho cha kulelea yatima wa Ebola kinachoendeshwa na asasi ya
Uingereza, nje kidogo mwa mji mkuu wa nchi ya Sierra Leone, Freetown.
Kufuatia tukio hilo watoto 33 pamoja
na watumishi saba wa kituo hicho cha St George Foundation wamewekwa
chini ya karantini tangu marehemu Baker abainike kuwa na virusi vya
Ebola.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni