.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 26 Februari 2015

MWANAMUZIKI CHIDI BENZ AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI JELA

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama 'Chid Benz' leo amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa.

Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi yenye tahamani ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Awali Februari 18 Chidi Benz alikiri mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema mashtaka matatu yanayomabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kukutwa na dawa za kulevya, kifuu cha nazi na kijiko vinavyotumika kuvutia ama kunusa dawa hizo za kulevya.

Rapa huyo amefanikiwa kulipa faini hiyo ya shilingi laki 9, na kuachiwa huru baada ya mama yake mzazi kuilipa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni