.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 26 Februari 2015

PUSH MOBILE, UN , WIZARA KUKABILI EBOLA


FullSizeRender
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia ujumbe mfupi maneno katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid.(Picha na Umoja wa Mataifa).

                                                                               Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya simu ya Push Mobile imetiliana saini na serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu ugonjwa hatari wa ebola.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini hapa kampuni hiyo ya simu imesema kupitia ushirikiano huo kampuni hiyo ya simu itaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola.

Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, serikali na wadau wake watatoa taarifa kuhusu ugonjwa huo wanapohitajika.

Watanzania wanaweza kupata habari za ugonjwa huo kwa kuandika neno EBOLA kwenye namba 15774 na kupata taarifa za ugonjwa huo bure bila kutozwa gharama.
IMG_8005
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento wakionyesha hati za makubaliano ya ushirikiano huo.

Wakitia saini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento amesema kwamba kama Ujumbe mfupi unaweza kuokoa maisha kampuni yake iko tayari kushiriki katika kampeni hiyo.

“..Teknolojia inatoa fursa ya pekee ya kuandaa jamii dhidi ya ugonjwa wa ebola na nini cha kufanya ukitokea. Kupitia ushirikiano huo kati yetu na Umoja wa Mataifa na Wizara ya afya na ustawi wa jamii tunaamini tutasaidia wananchi kuelekewa na kutambua dalili za ebola, kuzuia na kudhibiti maambukzi ya virusi vya ebola”, alisema Manento.

Katika miezi iliyopita vifo kutokana na ugonjwa wa ebola vimefikia 9000 huku vifo vingi vikitokea katika nchi za Liberia, Sierra Leone, na Guinea. Hadi sasa watu 23,000 wameelezwa kukumbwa na ugonjwa.
photo(36)
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento kwa pamoja wakionyesha ujumbe mfupi wa maneno unaotoa elimu ya ugonjwa wa ebola kwa baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria hafla hiyo.

Tanzania ikiwa na watumiaji wa simu milioni 30 na kufanya uwezekano wa kufikia watu hao kuwa ni asilimia 68.

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez amesema teknolojia ya simu itasaidia sana kuleta uelewaq wa ugonjwa huo miongoni mwa Watanzania.

“Mlipuko wa ugonjwa wa ebola umepungua sana Afrika magharibi na Tanzania haijawahi kukumbwa na ugonjwa huo.

Lakini kunahitajika mtu mmoja tu kuwa na ugonjwa huo na kuleta mashaka makubwa katika maisha ya watu nchini. Tukiungana na sekta binafsi, Umoja wa mataifa unaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kuongeza upeo wa utayari katika kukabiliana na Ebola
FullSizeRender (4)
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid akimshukuru Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano huo. Kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni