.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 26 Machi 2015

NDUGU NA MARAFIKI WA ABIRIA 150 WALIOKUFA KWA AJALI YA NDEGE KUTUMBELEA ENEO LA AJALI

Ndugu na marafiki wa abiria 150 pamoja na watumishi wa ndege Germanwings waliokufa kwenye ajali, wanatarajiwa kutembelea eneo ilipoanguka ndege hiyo katika milima ya Alps nchini Ufaransa.

Shirika la ndege la Ujerumani la Lufthansa litapeleka ndege mbili maalum, moja ikitokea Barcelona na nyingine ikitokea Duesseldorf hadi Marseille, na baada ya hapo ndugu hao watasafirishwa kwa njia ya barabara.

Ripoti zimeeleza kuwa mmoja wa marubani wa ndege hiyo iliyoanguka alikuwa ameondoka katika chumba cha kuongozea ndege na hakuweza kurejea kusaidiana na mwenzake kabla ya ndege kuanguka.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni