.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 26 Machi 2015

UN KUAINISHA ENEO LA KUMBUKUMBU YA BIASHARA YA UTUMWA



KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amesema UN itaainisha eneo maalum na la kudumu mahususi kwa ajili ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara za utumwa zilizoendeshwa Bahari ya Atlantiki.

Ki-moon ametoa kauli hiyo kwenye hotuba yake maalum aliyoitoa leo kwenye tukio la kumbukumbu ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki.

Alisema sehemu hiyo maalum ya kumbukumbu itakayokuwa Jijini New York itatoa fursa kwa watu kutoka mataifa mbalimbali kufika eneo hilo na kujufunza mengi kupitia matukio yaliajiri nyuma kipindi cha utumwa.

Alisema kwa taasisi za imataifa ikiwemo UN itatoa fursa kuangalia mikakati yao katika utendaji wa kazi ili kuhakikisha heshima, uhuru na usawa kwa binadamu wote vinalindwa sehemu zote.

Alisema kwa mwaka huu maadhimisho ya kumbukumbu kwa biashara ya utumwa inawakumbuka zaidi wanawake ambao waliteseka na wengine hadi kuuwawa kutokana na biashara zautumwa. “…Wanawake wengi walipata mateso makubwa kutokana na biashara ya utumwa…walinyanyaswa, walitumika kimapenzi na walilazimishwa kuzaa na hata kuuza watoto wao bila kupenda…,” ilieleza taarifa ya Ki-moon.

Alisema biashara ya utumwa bado inaendelea kwa baadhi ya nchi na kutolea mfano kwa mataifa ya Syria na Iraq ambayo hadi leo maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wamekuwa wakitekwa kuteswa huku vijana na watoto wakinunuliwa na kutumika kwenye mapigano jambo ambalo ni utumikishaji mbaya.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi. Usia Nkhoma akiwasilisha mada kwa baadhi ya washiriki wa maadhimisho ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara zake zilizoendeshwa eneo la Bahari ya Atlantiki, yaliyofanyika Dar es Salaam leo aliikumbusha jamii kujifunza kupitia historia.

Alisema UN iliamua kutumia siku ya kumbukumbu kuweza kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala anuai yanayofanywa kinyume na haki za binadamu kumaliza chembe chembe za utumikiswaji.

Aidha katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance Francais wa jijini Dar es Salaam washiriki walipata kuona picha za maonesho kuzungumzia biashara ya watumwa pamoja na filamu anuai.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni