Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Mabalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha kuongea nao.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani anyoamtambulisha mbele ya mabalozi wa heshima na kwamba yeye Rais mstaafu ndiye aliyefanya mageuzi ya mfumo wa uchumi Tanzania tunaoendelea nao hivi sasa.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongea na Mabalozi wa Heshima kuwashukuru kwa kuipenda na kuitangazaTanzania nchini Marekani na kuwaasa wasichoke kwa wao wamekua chachu ya maendeleo ya nchi aipendayo Tanzania.
Mbalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi zinazotangaza Utalii na uwekezaji Tanzania wakimsuikiliza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Picha ya pamoja. Mayor De Andre Windom wa mji wa Highland Park jimbo la Michigan akipata picha na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimuaga Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi wakati walipokua waiondoka baada ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kumaliza kufunga kikao cha Mabalozi wa Heshima Ubalozini hapo. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni