.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 26 Aprili 2015

WATANZANIA WALIOKWAMA AFRIKA KUSINI WAREJEA NYUMBANI

Kundi la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet. 

Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.

MWISHO.

                                                                              Imetolewa na:
                                            Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
                                      Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
                                                                             25 Aprili 2015



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni