.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 29 Julai 2015

CCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAITAKA TUME KUONGEZA VIFAA ILI KUFANIKISHA ZOEZI

Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi alisema anawashukuru waandishi kwa ushirikiano waliounesha kwenye mkutano
wa kumtambulisha mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.

Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani
na Ubunge .

Katika mkutano huo ambao waandishi wengi walionekana kuwa na
shauku ya kutaka kujua maoni ya CCM juu ya kuondoka kwa Edward Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa
aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni