.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 1 Julai 2015

MWANAMUZIKI LOVY LONGOMBA AJIWEKA KARIBU NA GWEN STEFANI


Nyota wa muziki Lovy Longomba kutoka kundi la Longombaz ambao kwa sasa wapo Marekani, ameendelea kuonyesha uwezo wake katika jukwaa la muziki la kimataifa, kwa sasa akionekana kuwa karibu na mwanadada Gwen Stefani, studio kufanya kazi pamoja.

Lovy ambaye amekwishajitengenezea jina kwa kusuka ngoma ya Change My Life ya Iggy Azalea ambaye ni staa mkubwa kabisa, kwa nafasi hii mpya ya ukaribu wake na Gwen, tayari imekwishaonekana kuwa ni nafasi nyingine kubwa ya kuionyesha dunia uwezo wake.

Huu unakuwa ni mwaka wa 8 sasa kwa Longombaz tangu kuhama kutoka Kenya, ambapo Lovy ameendelea kufanya kazi kwa nguvu hasa kwa upande wa utayarishaji muziki, wakati ndugu yake Christian akijikita katika kutunza familia yake pamoja na shughuli nyingine.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni