.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 30 Julai 2015

ZANZIBAR YAANZA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUSAMBAZA NA KUPATA TAARIFA MADAWA VITUONI

Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa jinsi unavyofanyakazi zake kwa haraka, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la John Snow Incorporated (JSI) nchini, Deo Kimera akitoa nasaha zake kwa Viongozi na Maafisa wa Afya waliopata elimu juu ya matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa wa kielektroniki walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mshauri Mwandamizi kutoka Shirika la Misaada la Marekani USAID Kelly Hamblin akitoa shukran zake kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano yao ya kufanikisha Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa nchini, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akitoa shukrani zake kwa Shirika la John Snow Incorporated (JSI) kutokana na juhudi zao za kuwawezesha maafisa wa Afya wa Zanzibar kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa kwa njia ya kielektroniki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mfamasia kutoka Bohari Kuu Zanzibar Bi. Khadija Ali Shehe akielezea changamoto walizokumbana nazo wakati wa kutumuia mfumo wa Karatasi katika Usambazaji wa Madawa vituoni kabla ya kuzinduliwa Mfumo mpya wa kielectroniki hii leo
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Gombani Pemba Abdalla Mbaruk Saleh akitoa ushuhuda wa namna Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa unavyofanya kazi zake kwa haraka na ufanisi, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna katikati akizindua Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Kulia kwake ni Msimamizi wa taaluma kutoka Shirika la John Snow Incorporated (JSI) Anselm Namala ,na kushoto ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman. Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna kushoto akihutubia mara baada ya uzinduzi wa Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
 
                                                                                       Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni