.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 24 Novemba 2015

ANDY COLE ADHAMIRIA KUPONA TATIZO LA FIGO KUSHINDWA KUFANYAKAZI

Aliyekuwa mshambuliaji nyota wa timu ya Manchester United, Andy Cole, amedhamiria kupona tatizo la figo kushindwa kufanyakazi na anamatarajio ya kupona kabisa katika majira ya kiangazi.

Cole, 44, ambaye alitwaa makombe matano ya Ligi Kuu ya Uingereza na United kati ya 1995 na 2001, alibainika kuwa na tatizo hilo na anapatiwa tiba katika hospitali ya Manchester Royal Infirmary kwa wiki tatu zilizopita.

Maradhi hayo yamemfanya ajitoe katika mchezo wa kujitolea ulioandaliwa na shirika la UNICEF katika dimba la Old Trafford na kutoa taarifa kuelezea kwanini hatashiriki mchezo huo kwa mashabiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni