.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 24 Novemba 2015

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO, AMOS MAKALLA ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE WA KIA


Katika kikao cha menejimenti ya kampuni ya uendeshaji uwanja KADCO, mkuu wa mkoa ameupongeza uongozi kwa kuongeza ndege zinazotua na kuruka, uwezo wakujiendesha kwa kuwa na mapato mazuri na uwezo wa kudhibiti vitendo haramu vya madawa ya kulevya, usafirishaji nyara za serikali na ugaidi.
Pamoja na pongezi hizo mkuu wa mkoa ameagiza yafuatayo yatekelezwe;
 
1. Uwanja wa Kia usiwe njia ya wapitishaji ea madawa ya kulevya kwani kuruhusu hilo tunapoteza nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana
 
2. Uwanja wa Kia usiwe njia ya kutorosha nyara za taifa kwani kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya taifa na raslimali za taifa
 
3. Ameagiza menejimenti kuutangaza uwanja huo kimataifa ili uvutie wageni zaidi kuja kuona vivutio vya utalii tukivyonavyo na kufanya hivyo ni kuongeza pato la taifa
 
Aidha amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa umoja na kutanguliza uadilifu na uzalendo katika kutekeleza majukumu yao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni