.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Februari 2016

MABADILIKO YA VIWANJA STARTIMES KUNDI A


Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kumalizika siku ya Jumapili kwa michezo ya minne yak Kundi A kuchezwa katika viwanja tofauti ikianza saa 10 kamili jioni ili kufanya michezo hiyo kumalizika katika muda mmoja.

Mchezo kati ya Friends Rangers dhid ya Kiluvya United uliokuwa uchezwe katika uwanja wa Mabatini Mlandizi sasa utachezwa katika uwanja wa Azam Complex hamazi, huku mchezo kati ya Polisi Dar dhidi ya Polisi Dodoma uliokua uchezwe uwanja Shirika la Elimu kibaha sasa utachezwa uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Mechi za mwisho za Kundi A hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Friends Rangers FC vs Kiluvya United FC itachezwa uwanaj wa Azam Complex, Polisi Dar vs Polisi Dodoma (Mabatini), Ashanti United vs African Lyon (Karume) na Mji Mkuu vs Kinondoni Municipal Council FC zitachezwa Februari 14, 2016 katika viwanja husika

Mechi za Kundi B wikiendi hii hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes ni Kimondo Super SC vs Kurugenzi FC (Vwawa), Njombe Mji vs Lipuli FC (Amani), Ruvu Shooting vs Polisi Morogoro (Mabatini) na Burkina FC vs JKT Mlale (Jamhuri) zitachezwa Februari 13, 2016.


Mechi za mwisho za Kundi C hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Mbao FC vs Polisi Mara (CCM Kirumba), Polisi Tabora vs JKT Oljoro (Ali Hassani Mwinyi) na JKT Kanembwa vs Geita Gold (Lake Tanganyika) zitachezwa Februari 13, 2016 katika viwanja husika, huku Rhino Rangers wakicheza dhidi ya Panone FC siku ya Jumapili Februari 14, 2016.

Bodi ya Ligi (TPLB) inavikumbusha vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi hiyo, wasimamizi wa vituo kuwafahamisha kuwa mechi zote zinatakiwa kuchezwa kwa muda mmoja na kusisitiza kuwa mechi zote zitaanza saa 10 kamili jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.

Ni jukumu la Msimamizi na Kamishna kuhakikisha mechi yake inaanza katika muda uliotajwa (saa 10 kamili) bila kukosa. Utekelezaji wa maelekezo haya ni muhimu ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya upangaji wa matokeo vinavyoweza kujitokeza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni