.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Februari 2016

RAIS WA SUDANI KUSINI SALVA KIIR AMTEUA TENA RIEK MACHAR KUWA MAKAMU WA RAIS

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir amemteuwa tena mpinzani wake aliyekuwa muasi Riek Machar kuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo changa la Afrika kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa hilo.

Uteuzi huyo wa Machar uliotangazwa na televisheni ya taifa unachukuliwa kuwa ni sehemu ya makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza machafuko yaliyoduma kwa muda wa miaka miwili.

Sudani Kusini imekuwa katika machafuko tangu Desemba 2013, wakati mapigano kuibuka baina ya vikosi vitiifu kwa Kiir na wanajeshi wanaomuunga mkono Riek Machar, ambaye awali alikuwa makamu wa rais.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni