.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Februari 2016

SUPER D ATOA SADAKA WA NIABA YA BONDIA OMARI KIMWERI WA AUSTRALIA


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Deer Park, Victoria, Australia mtoto Mohamed Mussa wa Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33 Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Deer Park, Victoria, Australia mtoto Mohamed Mussa wa Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33 Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
  
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akitoa sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Australia kwa mtoto Kauthar Seif wa Madrasatul Nool Hudaa iliyopo mtaa wa mafia Dar es Salaam Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akigawa sadaka kwa niaba ya bondia Omari Kimweri anaefanya shughulizake Australia kwa watoto wa Madrasatul _Noor Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33 Sadaka hiyo imetolewa na Kimweri kwa ajili ya kuwakumbuka wenzake kwa kuwa yeye kazaliwa nchini Tanzania Picha na SUPER D BOXING NEWS

                                                                                               Na Mwandishi Wetu

BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia

Amewakumbuka ndugu zake kwa kutoa sadaka kwa watoto wa Madrasatul _Noor-Hudaa iliyopo kariakoo mtaa wa mafia namba 33

Akizungumza baada ya kutoa msaada uho kwa niaba ya Kimweri Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mfano uhu ni wakuigwa kwa mabondia mbalimbali

Kukumbuka kutoa sadaka japo kidogo kwa kipato wanachokipata kupitia mchezo wa masumbwi

Aliongeza kwa kusema kuna mabondia wengi nchini wanapata pesa nyingi kupitia mchezo wa ngumi lakini awawakumbuki watu wenye mahitaji mbalimbali


Kimweri anatalajia kucheza mpambano wake mwingine feb 26 akizipiga na Michael Camellion kutoka Philippinesa mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title utakaopigwa katika ukumbi wa

The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia

Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3

bondia huyo mtanzania anaefanya shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo huo atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA  kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana  na akishinda mchezo uho itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya feb 26

Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D'

Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga

ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake ndipo kilipozikiwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni