.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Februari 2016

WABUNGE WA UPINZANI AFRIKA KUSINI WATOLEWA BUNGENI RAIS ZUMA AKIHUTUBIA

Wabunge wa upinzani nchini Afrika Kusini wametolewa nje ya bunge wakati rais Jacob Zuma akilihutubia taifa kupitia bunge kutokana na kumkatiza mara kwa mara asihutubie.

Kiongozi wa wabunge wa chama cha mrengo wa kushoto cha Wapigania Uhuru wa Uchumi, amesema rais Zuma amelifanya taifa kuonekana ni mzaha.

Hotuba hiyo ilionekana kama ni sehemu ya rais Zuma, kupotezea kesi inayomkabili ya kutumia dola milioni 23 za umma kukarabati nyumba yake.

Kambi ya upinzani imekata uamuzi wa rais Zuma, kurejesha fedha hizo zilizotumika kwa ujenzi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni